Lango la Ajira na Ujasiriamali linalenga kutoa taarifa zinazosaidia kuwaunganisha watafuta ajira na wanaotaka kuwa wajasiriamali, hasa vijana na wanawake, na fursa na mipango iliyopo katika sekta hiyo ambazo huenda hazijulikani kwa wengi wanaotafuta ajira au wanaotaka kuanzisha biashara zao wenyewe.
Ni muhimu umma kuelewa ni huduma zipi zinapatikana, kundi lengwa ni lipi, nani anatoa huduma; jinsi gani, wapi na lini kupata huduma hiyo.
Tunawasilisha huduma katika makundi 3 yafuatayo :
- Kukuza ujuzi (mafunzo kazini, mafunzo ya ufundi stadi na ya kiufundi, n.k.)
- Huduma za ujasiriamali na maendeleo ya biashara (upatikanaji wa fedha, kujenga uwezo, n.k.)
- Hatua za soko la ajira (vituo vya huduma za ajira, huduma za ushauri wa taaluma, n.k.)
